Madaktari wa tiba ya maungo katika hospitali ya Rufaa ya Vihiga wamehoji kwamba gharama ya usafiri imeathiri kufanikisha kwa matibabu miongoni mwa wagonjwa wanaougua ugonjwa wa viungo vya mwili. Wito huu umejiri wakati wa kusherekea siku ya tibamaungo katika Hospitali ya Rufaa ya Vihiga ambapo madaktari waliandaa mafunzo maalum kwa wagonjwa wa viungo vya mwili ili kuwahamasisha jinsi ya kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo wakati wa kuugua. Hali hii ya gharama ya usafiri miongoni mwa wagonjwa ameathiri matibabu ya wagonjwa hao ikisababisha historia ya ugonjwa kutotambuliwa mapema ili waweze kupewa tiba mwafaka ifaayo na madaktari katika hospitali hiyo. Jerusa Ndenga ni mmoja wa madaktari katika hospitali ya Rufaa ya Vihiga ambaye ameomba usimamizi wa Hospitali kutenga maeneo maalum ya wagonjwa kufanyia mazoezi ili kufanikisha safari ya matibabu ya wagonjwa wanaougua viungo vya mwili.